YANGA YAFUKUZA MWIZI KIMYA KIMYA, YAIPIGA MAJIMAJI 4G

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Yanga imeendelea kuifukuza Simba kileleni mwa msimamo baada ya kuifunga Majimaji mabao 4-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo umewafanya mabingwa hao kufikisha pointi 37 wakiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya Simba ambao watashuka dimbani kesho kucheza na Mwadui FC.

Ajib akimtoka beki wa Maji Maji

Majimaji walicheza pungufu muda mrefu kufuatia mlinzi wake wa kati Mpoki Mwakinyuke kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 18 baada ya kuunawa mpira uliokuwa unaelekea wavuni.

Kiungo Papy Tshishimbi alifunga mabao mawili moja kwa penati dakika ya 20 na jingine kwa shuti nje ya 18 dakika ya 84.

Mabao mengine ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 29 na Emmanuel Martin dakika ya 44.

Bao la kufutia machozi la Majimaji lilifungwa na mshambuliaji Marcel Bonaventure kwa penati dakika ya 56 baada ya Said Makapu kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *