Yanga Yaifuata Simba Sportpesa

KLABU ya Yanga imekuwa ya pili kusaini mkataba na kampuni ya bahati nasibu ya SportPesa baada ya Simba kufuatia tukio la leo la kusaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya shilingi bilioni tano.

Mkataba huo ulisainiwa mbele ya Waandishi wa Habari huku viongozi kadhaa wa klabu hiyo pamoja na viongozi wa matawi wakishuhudia ambapo Makamu Mwenyekiti wao Clement Sanga alisema mkataba huo utakuwa na faida kubwa kwa mabingwa hao.

Yanga itakuwa ikipokea shilingi milioni 950 kwa mwaka kwa mujibu wa mkataba huo huku kiasi hicho kikiongezeka kwa asilimia tano kila mwaka.

PicsArt_05-17-12.36.35

Sanga alisema “Leo tumeingia mkataba mnono na SportPesa na tunaamini utatusaidia kwa kiasi kikubwa katika masuala ya kuendesha klabu hii katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Abbas Tarimba alisema dhamira yao ya kuwekeza katika soka la Tanzania ni kuziona timu za Simba na Yanga ambazo wameingianazo mkataba, zinafanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Leo tumeingia mkataba na timu nyingine ya Tanzania baada ya Simba ambayo ni Yanga hivyo msimu ujao itavaa jezi yenye nembo yetu kifuani. Moja ya malengo ya SportsPesa ni kuzifanya timu hizi kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali,” alisema Tarimba.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *