YANGA YASIKITISHWA NA MAAMUZI YA TARIMBA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesikitishwa na malalamiko yaliyotolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalum Tarimba Abbas kwenye vyombo vya habari na ameamua kujiuzulu.

Jana usiku Tarimba alitangaza kujiuzulu akiwa katika studio za Radio Uhuru akiwatuhumu baadhi ya viongozi kuwa ndio wanasababisha matatizo akiwemo Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga.

Mwenyekiti wa matawi wa klabu hiyo, Bakili Makele amesema Tarimba amefanya makosa makubwa kwenda Redioni akiwa na Mohammed Msumi ambaye alienda Mahakamani kitu ambacho kimeushtua uongozi.

Bakili ameongeza kuwa baada ya kujiuzulu kwa Tarimba mambo mengine yote yanaendelea vizuri na usajili unafanyika kama kawaida na maadalizi ya mechi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia yako vizuri.

“Uongozi umesikitishwa na maneno ya Tarimba, umeushutumu uongozi kwenye vyombo vya habari na alikuwa na uwezo wa kuja klabuni ili kama kuna tatizo liwekwe sawa lakini amekimbilia katika vyombo vya habari.

“Kibaya zaidi ameenda Radio Uhuru ambayo anajua siku zote inatangaza mabaya tu ya Yanga tena akiwa na Msumi ambaye alijitoa Yanga kwa kwenda Mahakamani hilo ni jambo ” alisema Bakili.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *