YANGA YAWAFANYIA KITU MBAYA WALIYOIBANIA SIMBA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stand iliibana Simba siku chache zilizopita kwa kuilazimisha sare ya mabao 3-3 katika uwanja huo huo wa Taifa na kuifanya kuzidi kusogelewa na Yanga.

Yanga imefikisha pointi 46 sawa na Simba ambao wana mchezo mmoja mkononi lakini wakiendelea kubaki kileleni mwa msimamo kutokana na uwiano wa mabao ya kufunga.

Yanga walipata bao la mapema dakika ya sita la kujifunga la mlinzi Ally Ally aliyekuwa akitaka kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Yusuph Mhilu.

Ibrahim Ajibu aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 11 akipokea pasi kutoka kwa Maka Edward baada ya kugongeana pasi katika eneo la hatari la Stand.

Stand hawakuonekana wakiwa na madhara sana kwenye lango ya Yanga kipindi cha kwanza wakifanya mashambulizi machache langoni mwa Yanga ambayo yaliokolewa na walinzi.

Stand ilirudi kwa kasi kipindi cha pili kwa kuliandama lango la Yanga ingawa mlinda mlango Youthe Rostand alikuwa kikwazo kikubwa kwa Wapiga debe hao.

Dakika ya 84 Vitalis Mayanga aliipatia Stand bao la kufutia machozi kabla ya Obrey Chirwa kufunga la tatu dakika moja baadae.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *